Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Urusi yaingilia kati sakata la mapenzi ya jinsia moja Kenya

Shinikizo Laongezeka Kwa Rais Ruto Kutangaza Dharura Ya Kitaifa Urusi walaani uungwaji mkono wapenzi wa jinsia moja Kenya

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Ubalozi wa Urusi nchini Kenya umekuwa ukionesha kuunga mkono msukumo wa viongozi wa eneo hilo kulaani kile wanachodai ni kukuza utamaduni wa LGBT.

Hii inafuatia uamuzi wa wiki iliyopita wa Mahakama ya Juu ambao unaruhusu jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja kusajili vikundi vya kushawishi nchini Kenya.

Wafuasi hao wanasema majaji hao waliamini kuwa wanadai haki ya kujumuika kama inavyopewa raia wote, lakini uamuzi huo ulipata upinzani mkubwawapinzani, akiwemo Rais William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga, waliwashutumu majaji hao kwa kuendeleza maadili "yasiyo ya Kiafrika".

Wengi walitafsiri tofauti hukumu hiyo na kuona ni kama kuipa jumuiya ya LGBT uhuru wa kufunga ndoa nchini Kenya.

Moja ya ujumbe wa ubalozi huo ulisema: "Vladimir#Putin: "Kadri nitakavyokuwa rais, tutakuwa na ''baba'' na ''mama''".

Mwingine akasema: "Magharibi taikuja kwa zaidi. Maadili ya kimapokeo yatalindwa, vinginevyo ubinadamu utaangamia."

Chanzo: Bbc