Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Urusi yaikasirisha serikali ya Guinea baada ya serikali kuvunjwa

Urusi Yaikasirisha Serikali Ya Guinea Baada Ya Serikali Kuvunjwa Urusi yaikasirisha serikali ya Guinea baada ya serikali kuvunjwa

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Wanajeshi wa Guinea wameandamana hadi kwa balozi wa Urusi baada ya ubalozi wake kuripotiwa kuonya kuhusu uwezekano wa machafuko katika mji mkuu wa Conakry.

Onyo hilo lilitolewa baada ya kiongozi wa junta Kanali Mamady Doumbouya kuvunja serikali siku ya Jumatatu, na kuamuru kufungwa kwa mipaka yote.

Balozi Alexey Popov aliomba msamaha kwa junta kwa kile alichokiita kutokuelewana, vyombo vya habari vya Guinea viliripoti.

Kanali Doumbouya alichukua mamlaka baada ya mapinduzi ya 2021.Alivunja serikali yake siku ya Jumatatu bila kutoa maelezo yoyote.

Pia aliamuru kukamatwa kwa pasipoti za mawaziri waliofutwa kazi, na akaunti zao za benki kufungiwa.Vyombo vya habari vya Guinea viliripoti kuwa uamuzi wa Kanali Doumbouya ulipelekea ubalozi wa Urusi nchini Guinea kuwashauri raia wa Urusi kuwa waangalifu kwani kunaweza kutokea machafuko katika mji mkuu wa jimbo hilo la Afrika Magharibi, Conakry.

Junta ilijibu kwa hasira, na afisa katika wizara yake ya mambo ya nje kumwita Bw Popov kwenye mkutano.

"Nilieleza kuwa ilikuwa ni kutoelewana, tafsiri ya uongo ya kile kilichochapishwa. Tangazo hilo lilichapishwa kwa Kirusi pekee kwa raia wa Urusi," Bw Popov alinukuliwa na televisheni na redio inayomilikiwa na serikali ya Guinea.

Serikali ilikubali msamaha huo, huku Bw Popov akisema kisa hicho hakitaathiri uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Guinea ni mojawapo ya makoloni kadhaa ya zamani ya Ufaransa huko Afrika Magharibi ambayo yamekumbwa na mapinduzi katika miaka ya hivi karibuni.Wanajeshi, ambao walichukua mamlaka katika Mali, Niger na Burkina Faso wameegemea kwa Urusi, huku wakiwa na chuki dhidi ya Ufaransa na kambi ya kanda ya Afrika Magharibi, Ecowas.Lakini Kanali Doumbouya amejaribu kudumisha uhusiano mzuri na pande zote.

Ameahidi kufanya uchaguzi ili kurejesha utawala wa kidemokrasia ifikapo mwisho wa 2024.Utawala wa kijeshi ulipiga marufuku maandamano yote mwaka wa 2022 na umewaweka kizuizini viongozi kadhaa wa upinzani, na wanachama wa mashirika ya kiraia.

Kanali Doumbouya alimpindua Rais Alpha Condé mnamo Septemba 2021, akisema jeshi lilikuwa na chaguo dogo ila kunyakua mamlaka kwa sababu ya kukithiri kwa rushwa, kutozingatia haki za binadamu na usimamizi mbovu wa kiuchumi.

Chanzo: Bbc