Vikosi vya Kijeshi mashariki mwa Libya vinasema kuwa wamepata takriban tani 2.5 za madini ya Uranium, karibu mwa mpaka wa Nchi hiyo na Chad, ambayo yaliripotiwa kupotea na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki
Mnamo Machi 16, 2023, Shirika hilo lilitoa tangazo la tahadhari baada ya wakaguzi wake kukosa madini hayo katika eneo yalimokuwa yamehifadhiwa, wakihofia hatari ya mionzi na kutengenezwa silaha za nyuklia
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya nyuklia linasema kuwa linajaribu kutafuta karibu Tani 2.5 za madini ya 'Uranium' ambayo yametoweka katika eneo ambalo haliko chini ya udhibiti wa serikali ya Libya
Imeelezwa kuwa wakaguzi waligundua kuwa madumu 10 yaliyokuwa na madini hayo ambayo hutumika kutengeneza Silaha za Nyuklia hayaonekani katika ghala yalimokuwa yamehifadhiwa
Wakaguzi hao wanahofia kuwa Uranium hiyo inaweza kusababisha hatari ya kimionzi na wasiwasi wa usalama wa nyuklia