Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upinzani wataka uchunguzi wa nyumba za mawaziri

Afrika Kusibi Srtf Upinzani wataka uchunguzi wa nyumba za mawaziri

Mon, 22 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama Kikuu cha Upinzani cha Democratic Alliance (DA) nchini Afrika Kusini kimeomba mamlaka ya kupambana na Rushwa na Ufisadi kuchunguza mikataba inayodaiwa kuwa na gharama kubwa kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za Mawaziri zinazotajwa kuwa za anasa.

Ni baada ya Serikali kubainisha kuwa kati ya 2019 na 2022, ilitumia karibu USD Milioni 5 sawa na Tsh. Bilioni 11.8 kwa ajili ya matengenezo ya nyumba za watumishi wa umma, ambapo inakadiriwa kuwa taa moja iligharimu karibu USD 1,000 katika moja ya nyumba za Mawaziri jijini Pretoria.

Pia, takriban USD 70,000 zilitumika kukarabati majiko huku USD Milioni 2.5 kwa ajili ya majenereta katika nyumba za Mawaziri, wakati ambao Raia wengi wanapambana na changamoto za kukatika kwa umeme mara kwa mara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live