Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upinzani washinda urais Guinea Bissau

90526 Guinea+pic Upinzani washinda urais Guinea Bissau

Thu, 2 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bissau.  Kiongozi wa upinzani Umaro Sissoco Embalo ameshinda urais nchini Guinea Bissau baada ya kupata asilimia 53.55 ya kura zote, Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo (CNE) imetangaza.

Mshindani wake Domingos Simoes Pereira, kiongozi wa chama tawala (PAIGC) amepata asilimia 46.45 katika uchaguzi huo wa marudio.

“Ninamtangaza Umaro Sissoco Embalo kuwa mshindi wa uchaguzi huu wa marudio,” amsema Rais wa CNE, Jose Pedro Sambu

Embalo anachukua uraia kutoka kwa Jose Mario Vaz aliyechukua madaraka mwaka 2014 akiwa na matumaini ya kuituliza nchi hiyo ambayo imeandamwa na mapinduzi na mauaji ya viongozi tangu ilipopata uhuru mwaka 1974.

Lakini katika kipindi hicho ilikabiliwa na nguvu ya Bunge.

CNE imesema watu waliojitokeza kupiga kura walikuwa asilimia 72.67, sawa na ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza wa Novemba 24, ambapo Pereira alishinda kwa asilimia 40.1 dhidi ya asilimia 28 za Embalo. Embalo (47) ni Brigedia generali wa zamani ambaye hupendelea kufaa kiremba kichwani. Kama alivyo Pereira, yeye pia ni waziri mkuu mstaafu akiwa amefanya kazi na Rais Vaz kati ya mwaka 2016 na 2018, kabla ya kuwakilisha chama cha Madem, kilichoungwa na waasi kutoka cha tawala cha PAIGC.

Alipambana kupunguza pengo la kura za raundi ya kwanza, akijionyesha kama mtu atakayeiunganisha nchi, akiungwa mkono na wagombea walioenguliwa akiwamo Vaz.

Chanzo: mwananchi.co.tz