Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upinzani nchini Ghana wapinga ombi la kubadilisha tarehe ya uchaguzi

Upinzani Nchini Ghana Wapinga Ombi La Kubadilisha Tarehe Ya Uchaguzi Upinzani nchini Ghana wapinga ombi la kubadilisha tarehe ya uchaguzi

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Mgombea urais wa upinzani nchini Ghana John Mahama amepinga pendekezo la uchaguzi mkuu kurejeshwa hadi Novemba kuanzia Desemba mwaka huu.

Tume ya Uchaguzi (EC) ilisema pendekezo hilo lililotolewa awali na vyama vya siasa, lililenga kutoa muda wa kutosha kwa tume hiyo kusimamia vyema shughuli zake, hasa inapotokea marudio ya uchaguzi.

Hata hivyo, Bw Mahama, mgombeaji wa chama cha National Democratic Congress (NDC) alisema mabadiliko ya tarehe ya uchaguzi mkuu hayakuwezekana.

"Hatuamini kwamba hii inapendekezwa kwa nia njema," Bw Mahama alisema Jumamosi, akishutumu tume hiyo kwa kukosa kujitayarisha.

Rais huyo wa zamani aliitaka tume hiyo kuweka mambo yake sawa ili kuhakikisha uchaguzi wa kuaminika.

Kanisa la Waadventista Wasabato pia lilikuwa limeiomba tume hiyo kusogeza siku ya uchaguzi kutoka siku ya kawaida ya tarehe 7 Desemba kwa sababu Jumamos itakuwa i, siku yake ya ibada.

Tume hiyo pia inazingatia kuteua siku zote za uchaguzi kuwa sikukuu za kitaifa ili kusaidia kuongeza idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura.

Haijabainika iwapo mapendekezo hayo mapya yanahusishwa na ombi la kanisa.

Chanzo: Bbc