Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upinzani Kenya watoa wajumbe watano kabla ya mazungumzo ya amani

Upinzani Kenya Watoa Wajumbe Watano Kabla Ya Mazungumzo Ya Amani Upinzani Kenya watoa wajumbe watano kabla ya mazungumzo ya amani

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya umewataja wajumbe watano kabla ya mazungumzo ya amani na Kenya Kwanza.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya Rais Ruto kutangaza kuwa amekutana na mpinzani wake wa kisiasa, Raila Odinga.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Jumatatu Azimio ilisema kwamba ujumbe wake utaongozwa na Kalonzo Musyoka na kujumuisha kiongozi wa Wachache bungeni Opiyo Wandayi na kiongozi wa Chama cha DAP Eugene Wamalwa.

Wengine ni pamoja na Seneta wa Nyamira Senator Okon'go Omogeni na Mbunge wa Malindi Amina Mnyazi.

Gharama ya juu ya maisha, mapitio ya Uchaguzi Mkuu wa 2022, na upangaji upya wa tume ya uchaguzi nchini Kenya (IEBC) kwa pande mbili ni baadhi ya masuala ambayo ujumbe wa Azimio unapanga kuibua.

Viongozi hao wawili wanasemekana kuwa walifanya mazungumzo ya kwanza ya mfululizo wa kutatua tofauti kati ya serikali ya Kenya Kwanza na upinzani, iliyopatanishwa na Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo.

Baadhi ya Wakenya wanataona mazungumzo ya hivi punde kama iwapo yatafanyika huenda yakaashiria mwisho wa mzozo wao wa kisiasa baina ya serikali na upinzani na kutangaza duru mpya ya mazungumzo ya pande mbili.

Chanzo: Bbc