Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upinzani Jamhuri ya Afrika ya kati: Kura ya maoni ilisusiwa na wapiga kura

Upinzani Jamhuri Ya Afrika Ya Kati: Kura Ya Maoni Ilisusiwa Na Wapiga Kura Upinzani Jamhuri ya Afrika ya kati: Kura ya maoni ilisusiwa na wapiga kura

Fri, 4 Aug 2023 Chanzo: VOA

Chama cha upinzani nchini Jamhuri ya Afrika ya kati Alhamisi kilikemea vikali kura ya maoni ya mwishoni mwa juma lililopita, ambayo itamruhusu Rais Faustin Archange Touadera kuwania muhula wa tatu.

Vyama vikuu vya upinzani, mashirika ya kiraia na waasi , wote waliwaomba wapiga kura kususia kura hiyo ya maoni ambayo ilifanyika siku ya Jumapili.

Kiongozi wa upinzani Crepin Mboli-Goumba aliitaja kura hiyo ya maoni kuwa “mchakato uliofeli kwa uchungu” na kusema idadi ya wapiga kura ilikuwa ndogo, sawa na “asilimia 10 hadi asilimia 13” ya wapiga kura.

“Kura hii ilikuwa ya aibu kwa sababu Bangui ilionekana kama mji usiokaliwa na watu”, Mboli Goumba aliuambia mkutano wa waandishi wa habari katika mji mkuu Bangui.

Chama kikuu cha waasi, The Coalition of Patriots for Change, kilisema vituo vya kupigia kura havikuwa na watu, karibu nchi nzima.

Ulisema idadi ya wapiga kura “haiwezi kuzidi asilimia 5” na kumshtumu rais Touadera kujaribu”kuangamiza demokrasia na utawala wa sheria” Jamhuri ya Afrika ya kati, ambayo imekumbwa na mapinduzi kadhaa katika historia yake.

Naibu spika wa bunge na msemaji wa walio wengi bungeni Evariste Ngamana alisema siku moja baada ya kura hiyo kwamba idadi ya wapiga kura ilikuwa asilimia 70, akidai kwamba “ watu walijitokeza kupiga kura kwa wingi.”

Chanzo: VOA