Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upinzani Afrika Kusini waweka mabango ya ubaguzi wa rangi nchi nzima

Sa Pic Chama cha Upinzani SA chaweka mabango ubaguzi wa rangi nchi nzima

Thu, 7 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama Kikuu cha Upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance DA, kimeweka mabango katika maeneo ya mengi ya mji nchini humo yakionesha kupinga mauaji ya raia yaliyotokea wakati wa machafuko makubwa ya mwezi Julai, 2021.

Machafuko hayo ambayo yalichochewa na ubaguzi wa rangi yalizuka mara baada ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma kuwekwa gerezani tarehe 8 Julai, 2021 huku yakihusiha raia wenye asili ya kihindi walioanzisha vikosi vya ulinzi ili kuweza kulinda mali zao ambazo kwa wakati huo zilikuwa hatarini kuporwa na waandamanaji na wafuasi wa Zuma.

Machafuko hayo yalipelekea mauaji ya watu 36 huku raia hao wa kihindi wakilaumiwa kuhusika moja kwa moja na mauaji hayo.

Mabango hayo yaliyo zagaa katika miji karibu yote nchini humo yanasomeka yakiwa na ujumbe " Chama cha ANC kimewaita nyie Wabaguzi, ila sisi DA tunawaita Mashujaa"

Mpaka sasa mabango hayo yanakoselewa sana kuwa yanawagawa watu na kuchochea ubaguzi, kwani vitendo vilivyofanywa na watu hao vilikuwa kinyume na misingi ya haki za binadamu.

Nacho Chama tawala nchini humo cha National Congress ANC, kimesema kuwa mabango hayo yanatia aibu kwani yanachochea ubaguzi wa rangi.

"Hivi ndivyo DA walivyoishiwa sera, wamekufa kisiasa" amesema Msemaji wa ANC Nhlakanipho Ntombela.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live