Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upigaji kura waendelea Chad

Upigaji Kura Unaendelea Chad Huku Zoezi Likicheleweshwa Katika Baadhi Ya Maeneo Upigaji kura unaendelea Chad

Mon, 6 May 2024 Chanzo: Bbc

Upigaji kura umeanza katika uchaguzi wa rais wa Chad, hatua kubwa inayopelekea kumalizika kwa kipindi cha mpito cha miaka mitatu nchini humo.

Upigaji kura huo ulikumbwa na ucheleweshaji, na kufunguliwa saa moja baada ya muda uliopangwa katika baadhi ya maeneo.

Rais wa mpito Mahamat Déby alianza zoezi hilo kwa kupiga kura yake katika mji mkuu wa N'Djamena.

Alisema anajivunia kutimiza ahadi yake ya kuheshimu tarehe ya mwisho ya "uchaguzi ambao utaashiria kurejea kwa utaratibu wa kikatiba."

"Ni juu ya watu wa Chad kupiga kura kwa wingi na kuchagua rais wao," aliongeza.

"Tutapiga kura, ni jukumu letu… hata kama itachukua muda," alisema mpiga kura ambaye alisimama kwenye foleni ndefu akisubiri zamu yake ya kupiga kura.

Wapiga kura milioni nane wanamchagua rais kutoka miongoni mwa wagombea 10, akiwemo kiongozi wa kijeshi Déby na waziri mkuu, Succès Masra.

Matokeo ya awali yanatarajiwa kufikia tarehe 21 Mei, lakini duru ya pili inaweza kufanyika mwezi Juni ikiwa hakutakuwa na mshindi wa moja kwa moja katika duru ya kwanza ya uchaguzi.

Chanzo: Bbc