Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upendo wa agape! Wachumba wafunga ndoa wodini

Ndoa Hospitali Ms Upendo wa agape! Wachumba wafunga ndoa wodini

Fri, 30 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali moja nchini Nigeria imefurahia kwa waandaaji wa harusi kwa mara ya kwanza tangu kuasisiwa kwa hospitali hiyo, kufunga ndoa wodini.

Ndoa hiyo ilifungwa katika moja ya wodi za kulaza wagonjwa ambapo bwana harusi ndiye alikuwa amelazwa ila hilo halikuwa kizingiti cha kuzuia mwanamke kufunga naye ndoa akiwa bado mgonjwa kitandani.

Bwana harusi aliketishwa katika kiti cha magurudumu cha kusukumwa huku bibi harusi akiwa amevalia shela jeupe tayari kula kiapo cha pingu za maisha.

Katika [posti ya hospitali hiyo yenye jina la Evercare Hospital Lekki kwenye Instagram wametandaza picha na video za tukio hilo.

“Tulifanya harusi yetu ya kwanza kabisa ya Evercare. Hongera kwa wanandoa wapya kwa tukio hili muhimu na tunawatakia upendo wa milele na furaha ya ndoa,” posti zao zimesomeka.

Hafla maalum ya wanandoa hao ilishuhudiwa na wageni wachache ambapo mwanaume, akiwa kwenye kiti cha magurudumu alikula kiapo cha ndoa na bibi harusi wake ambapo video ya tukio hilo imewafurahisha watu wengi mitandaoni.

Wengine walizua ubishi kwamba harusi hiyo haiwezi kuwa halali kwani kuna sehemu husika za kufanyika kwa harusi na hiyo yao ni mbwembwe tu za mitandaoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live