Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uongozi wa kijeshi nchini Niger unaishtumu Ufaransa

Uongozi Wa Kijeshi Nchini Niger Unaishtumu Ufaransa Uongozi wa kijeshi nchini Niger unaishtumu Ufaransa

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: Voa

Uongozi mpya wa kijeshi nchini Niger Jumatatu umeishutumu Ufaransa kutaka ‘kuingilia kati kijeshi’ ili kumrejesha madarakani Rais aliyeng’atuliwa Mohammed Bazoum, huku mivutano ikiongezeka kati ya Niger na Ufaransa, iliyokuwa mtawala wa kikoloni kwa Niger, na majirani zake.

Ufaransa ilijbu mara moja Jumatatu jioni huku waziri wa mambo ya nje Catherine Colonna akikanusha madai hayo na kuongeza kuwa “bado inawezekana” kumrejesha madarakani Bazoum.

Na katika ishara ya kuongezeka kwa mvutano wa kikanda, serikali za Mali na Burkina Faso zinazoongozwa na wanajeshi Jumatatu jioni zilionya kwamba uingiliaji kati wowote wa kijeshi nchini Niger utachukuliwa pia “kama tangazo la vita” kwa nchi zao zote mbili.

Bazoum, mshirika wa karibu wa nchi za magharibi ambaye kuchaguliwa kwake miaka miwili iliyopita kuliashiria kukabidhiana madaraka kwa njia ya amani kwa mara ya kwanza tangu uhuru wa Niger, aliondolewa madarakani tarehe 26 Julai na kiongozi wa kikosi cha ulinzi wa rais.

Mkuu wa kikosi cha ulinzi wa rais Jenerali Abdourahamane Tiani alijitangaza kuwa kiongozi, lakini madai yake yalilaaniwa kimataifa, na Jumuia ya uchumi ya nchi za Afrika magharibi(ECOWAS) ilimpa wiki moja kurudisha madaraka.

Chama cha Bazoum cha PNDS Jumatatu kilionya kwamba Niger iko katika hatari ya kuwa “utawala wa kidikteta na kiimla” baada ya watu kadhaa kukamatwa.

Jumatatu asubuhi, waziri wa mafuta na waziri wa madini walikamatwa, chama cha PNDS kilisema. Kiongozi wa kamati kuu ya kitaifa ya PNDS alikamatwa pia.

Chanzo: Voa