Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unyama wa polisi wakati wa kafyu na habari zingine za kusisimua wiki hii

Ddb15b942f21bc0b Unyama wa polisi wakati wa kafyu na habari zingine za kusisimua wiki hii

Thu, 22 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kila siku ya wiki, TUKO.co.ke inakupakulia kwa mukhtasari matukio na habari muhimu zilizogonga vichwa vya habari wiki hii ili ukapate kufahamu kwa upana na utendeti mambo yalivyo ulimwenguni.

1. Penzi Hatari: Mshukiwa Asema Picha ya Dume Mwingine Ilimfanya Amuue Mpenziwe

Evan Karani, 38, alikiri kuwa alimuua aliyekuwa mpenziwe wa siri Catherine Nyokabi baada ya kusaliti penzi lao.

Kulingana na makachero wanaofuatilia kisa hicho, Karani alisema wamekuwa wapenzi na Nyokabi kwa miaka minne.

2. Wakenya Wakabili Polisi Waliofunga Thika Road Baada ya Kafyu Kufika

Wakazi wa Nairobi waliokuwa wamechelewa nje na masaa ya kafyu kufika walijipata pabaya baada ya polisi kufunga barabara ya Thika Road.

Polisi waliokuwa katika kizuizi walisema waliokuwa wamechelewa watalazimika kulala kwenye magari yao barabarani.

Ni hatua iliyozua msongamano mkubwa wa magari kwenye barabara hiyo huku waliofungiwa wakiteta kuhusu ukatili wa polisi na serikali wanayohudumia.

3. KCPE 2020: Wanafunzi wa Kike kutoka Shule za Umma Wawika, Wawabwaga Wenzao wa Kiume

Wanafunzi watatu wa kike kutoka shule tofauti za umma walijinyakulia nafasi za kwanza katika mtihani wa kitaifa wa darasa la nane (KCPE) wa mwaka huu.

Mwanafunzi aliyeibuka mshindi katika mtihani wa kitaifa wa darasa la 8 mwaka huu alitoka katika shule ya msingi ya Kari- Mwaili.

Faith Mumo alijizolea alama ya 433 kwa jumla ya alama 500.



4. George Floyd: Aliyekuwa Polisi Derek Chauvin Akutwa na Hatia ya Mauaji Kufuatia Uamuzi wa Mjaji

Afisa wa zamani wa kituo cha Minneapolis mjini Minnesota aliyeshtumiwa kwa kumuua Mmarekana mweusi George Floyd, Derek Chauvi amepatikana na hatia ya mauaji.

Chauvin mwenye umri wa miaka 45, alinaswa kwenye video akiwa amepiga goti kwenye shingo la Floyd kwa zaidi ya dakika tisa.



5. Mhubiri Tanzania Atoa Utabiri wa Utata Kuhusu Kenya, Asema Taifa Linapaswa Kuomba Sana

Mhubiri wa Kitanzania aliyetambuliwa kama Nabii Rolinga amevutia Wakenya baada ya kutoa utabiri wa kuzua wasiwasi kuhusiana na taifa.

Mtumishi huyo wa Mungu alisema aliiona bendera ya Kenya ikizama baharini, lakini rais Uhuru Kenyatta alikuwa ameketi kitako bila kujali wala kufanya lolote kuiokoa.

6. Mnakula Haramu: Matiang'i na Mawaziri Wengine 8 Waambiwa wako Afisini Kinyume cha Sheria

Mahakama Kuu imeamua kuwa mawaziri tisa akiwemo Waziri Fred Matiang'i wanashikilia nyadhifa hizo kinyume cha sheria.

Jaji Antony Mrima alisema mawaziri tisa katika serikali ya Jubilee hawakupigwa msasa na Bunge kuongoza wizara hizo katika muhula wa pili wa Rais Uhuru Kenyatta



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke