Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umoja wa mataifa wasikitishwa na mauaji ya watu 40 Burkina Faso

Umoja Wa Mataifa Wasikitishwa Na Maaji Ya Watu 40 Burkina Faso Umoja wa mataifa wasikitishwa na mauaji ya watu 40 Burkina Faso

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Umoja wa Mataifa umesema umesikitishwa na mauaji ya makumi ya raia yaliyofanywa na wapiganaji wa Kijihadi kaskazini mwa Burkina Faso siku ya Jumapili.

Umesema idadi kubwa ya wapiganaji kutoka kundi linalojulikana kwa jina la JNIM, wameshambulia kambi ya kijeshi, nyumba na kambi za watu waliokimbia makazi yao katika mji wa Djibo na kuua takriban raia 40.

Hapo awali jeshi lilithibitisha kuwa mamia ya watu wenye silaha walijaribu kupenya kambi yake ya kijeshi katika eneo hilo.

Burkina Faso inapambana na waasi wa kijihadi waliosambaa kutoka nchi jirani ya Mali mwaka 2015

Nchi hiyo inatawaliwa na serikali ya mpito iliyowekwa kufuatia mapinduzi ya kijeshi mwaka jana.

Chanzo: Bbc