Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umoja wa Ulaya washutumu vitendo vya mateso Uganda

Uganda Mateso Umoja wa Ulaya washutumu vitendo vya mateso Uganda

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Ulaya na Marekani zameshtumu hatua ya mwendelezo wa vitendo vya mateso na ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyofanywa na vyombo vya usalama.

Kanda ya video ikonyesha makovu yaliyojaa mgongoni mwa mwandishi Kakwenza Rukirabashaija imepokelewa na raia wa Uganda kwa hisia mseto za hasira, huzuni na huruma.

Mwandishi huyo ambaye kwa sasa anakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya mtandao kwa kumvunjia heshima rais Yoweri Museveni na mwanawe Jenerali Muhoozi Kainerugaba alikamatwa na kuzuiliwa kwa wiki kadhaa kabla ya kufikishwa mahakamani na kisha kuachiwa kwa dhamana.

Lakini hii yote ilikuwa baada ya mwito na vilio kutoka ndani na nje ya Uganda mwandishi huyo wa vitabu viwili maarufu vya kisiasa aachiwe. Mwandishi huyo amesimulia hivi madhila yake akiwa mikononi mwa vyombo vya usalama.

Ujumbe wa Ulaya nchini Uganda umesambaza taarifa ukilaani vikali mienendo ya kuwatesa raia na pia kukiuka haki zao za kikatiba kwa kutowafikisha mbele ya sheria kwa wakati stahiki.

Ujumbe huo umetaja vyombo vya usalama ikiwemo polisi na majeshi kwa kuwatisha na kuwahujumu raia pamoja na wanahabari kuwa mienendo ya kikatili siyostahili katika jamii iliyostarabika na kudai kuzingatia utawala wa kidemokrasia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live