Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umoja wa Ulaya waanza hatua za kuiwekea vikwazo serikali ya kijeshi ya Niger

Umoja Wa Ulaya Waanza Hatua Za Kuiwekea Vikwazo Serikali Ya Kijeshi Ya Niger Umoja wa Ulaya waanza hatua za kuiwekea vikwazo serikali ya kijeshi ya Niger

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Umoja wa Ulaya umeanza hatua za kuwawekea vikwazo wanachama wa utawala wa kijeshi wa Niger, miezi mitatu baada ya kuchukua mamlaka katika mapinduzi.

Baraza la EU lilitangaza Jumatatu kwamba "limepitisha mfumo" ambao utaliruhusu kuweka vikwazo dhidi ya "watu binafsi na vyombo vinavyohusika na vitendo vinavyotishia amani, utulivu na usalama wa Niger".

Baraza hilo pia lilisema kuwa vikwazo hivyo vitawekewa watu binafsi ambao wanahujumu utaratibu wa kikatiba wa Niger, demokrasia au utawala wa sheria, pamoja na watu binafsi wanaohusika naukiukaji wa haki za binadamu.

Vikwazo hivyo vitajumuisha marufuku ya usafiri, kufungia mali na kupiga marufuku utoaji wa fedha kwa watu waliowekewa vikwazo.

"Kwa uamuzi wa leo, EU inaimarisha uungaji mkono wake kwa juhudi za Jumuiya ya Afrika Magharibi, Ecowas na kutuma ujumbe wazi: mapinduzi ya kijeshi yana gharama," mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell alisema.

EU, hata hivyo, ilisema kwamba itakubali msamaha wa kibinadamu kwa hatua za kufungia mali.

Hatua hiyo ya Ulaya inafuatia Niger kuwekewa vikwazo na Ecowas na kusitishwa kwa misaada na serikali ya Marekani.

Chanzo: Bbc