Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa linaanza kikao kikubwa cha wiki tano mjini Geneva kuanzia Jumatatu.
Baraza hilo linakuza haki za binadamu duniani kote na kuchunguza ukiukaji huo.
Linatarajiwa kuangazia vitendo vya Urusi nchini Ukraine. Ajenda hiyo pia inahusu madai ya uhalifu wa kivita nchini Ethiopia, na ukandamizaji wa wanawake nchini Afghanistan na Iran.
Baraza hilo pia litaziangalia Myanmar, Sudan Kusini, Korea Kaskazini na Belarus.
Hata hivyo, nchi wanachama ziliamua kutojadili madai ya dhuluma za China dhidi ya jamii yake ya Kiislamu ya Uyghur. Kikao hiki kitafunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.