Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa litafanya kikao cha dharura juu ya Ethiopia, huku kukiwa na taarifa za maafa zaidi katika jimbo la Tigray.
Kikao hicho cha Ijumaa, ambacho kiliombwa na Muungano wa Ulaya, kitaamua iwapo utateuliwa ujumbe wa kimataifa kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu ambao makundi ya haki za binadamu yanasema unaweza kuwa uhalifu wa kivita.
Mzozo katka jimbo la Tigyar uliibuka mwezi Novemba mwaka jana, wakati serikali ya Eritrea ilipotuma vikosi vyake ndani ya jimbo hilo kuzima mashambulio yaTigray People’s Liberation Front – baada ya wapiganaji wake kuteka ngome za jeshi la serikali kuu.
Ni mwezi uliopita tu Umoja wa Mataifa ulitoa ripoti ya kurasa 100 iliyoelezea kwa kila ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu katika Tigray, ikiwa ni pamoja na kufyatua makombora katika miji, kuwauwa raia, na kusambaa kwa vitendo vya unyanyasaji wa kingono.
Wiki hii, mahsirika ya haki za binadamu ya kimataifa, Amnesty International na Human Rights Watch yaliainisha maafa zaidi ikiwa ni pamoja na kuwafunga mahabusu watu wengi, ukatili, kuwalazimisha watu wengi wa jamii ya Watigrayan kuhama makwao.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa hayana uwezo kwa kiasi kikubwa wa kuzifikia jamii nyingi ambazo zinakabiliwa na njaa kubwa.
Muungani wa Ulaya unasema baraza la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu lina jukumu la kuzuwia ukiukaji zaidi wa haki za binadamu, na kuhakikisha haki inapatikana kwa waathiriwa-nchi wanachama zinataka baraza hilo liwateuwe wachunguzi wa kimataifa.
Ethiopia imepuuzilia mbali hatua hiyo ikiitaja kuwa yenye uchochezi wa kisiasa.