Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umoja wa Afrika watuma maombi ya fedha Umoja wa Ulaya

EU SUED Umoja wa Afrika watuma maombi ya fedha kwa EU

Sun, 31 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchi za Afrika zimewataka wanachama wa Umoja wa Ulaya kuhamishia akiba zao ambazo hazijatumika katika Benki ya Dunia na IMF ii kuweza kusaidia mataifa yaliyoathirika na mlipuko wa ugonjwa Corona pamoja na madeni kutoka kwa wakopeshaji wa kimataifa.

Wamesema kuwa kufanya hivyo kutasaidia usambazaji wa chanjo kimataifa na kudumisha uhusiano mzuri kwa siku zijazo baina ya mataifa hayo na yale ya Ulaya.

"Tunatazamia kupata mgao wa feha hizo ambazo hazijatumika na mataifa ya Ulaya kupitia Benki ya Dunia na IMF ili kuongeza upatikanaji wa fedha kwa nchi zinazoendelea ambazo ndio wahitaji na nyingi zipo Afrika" Amesema Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Nchi za Afrika, Monique Nsanzabaganwa.

Nao Umoja wa Ulaya EU umesema kuwa utazisaidia nchi za Afrika kuinua uchumi wake kwa kupunguza madeni wanayodaiwa na wakopeshaji wakuu wa kimataifa.

"Sisi (EU) hatuzidai nchi za Afrika kwa ukubwa, tunafanyakazi kwa bidii ili kuweza kuongeza mgao huu wa fedha utakao saidia nchi nyingi za Afrika" Amesema Muwakilishi wa EU Josep Borrell.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live