Umoja wa Afrika umesisitiza msimamo wake wa kutovumilia mabadiliko ya utawala wa kidemokrasia katika bara hilo.
Katika siku ya mwisho ya mkutano wa AU uliofanyika mjini Addis Ababa, Umoja huo ulisema utaendelea kuzisimamishwa kwa Burkina Faso, Guinea, Mali na Sudan - ambazo zote zinatawaliwa na viongozi wa kijeshi kufuatia mapinduzi.
Kamishna wa masuala ya kisiasa, Bankole Adeoye, alisema AU iko tayari kusaidia nchi hizo kurejea katika utaratibu wa kikatiba na kusaidia demokrasia kuota mizizi.
Viongozi katika mkutano huo pia walikubali kuendelea na mipango ya mpango wa biashara huria ikiwa ni pamoja na karibu kila nchi barani Afrika.