Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umaarufu wa ANC wapungua katika uchaguzi wa mitaa Afrika Kusini

Cyril Ramaphosa?fit=754%2C409&ssl=1 Umaarufu wa ANC wapungua kabisa katika uchaguzi wa Afrika Kusini

Sat, 6 Nov 2021 Chanzo: BBC

Chama tawala nchini Afrika Kusini ,African National Congress (ANC) kimetumbukia chini zaidi katika umaarufu wake baada ya kupata chini ya asilimia 50 ya kura kwa mara ya kwanza katika historia ya kidemokrasia nchini Afrika Kusini. Matokeo ya uchaguzi wa mitaa uliofanyika Jumatatu yamekiacha chama cha Nelson Mandela kikiwa na majeraha ya kisiasa.

"Tunakula tembo huyu kidogo kidogo," ni maneno yaliyotolewa na Julius Malema, kiongozi wa chama cha tatu kikubwa cha Economic Freedom Fighters, huku picha ya wazi ikiibuka kuwa ANC ilikuwa ikipoteza uungwaji mkono kote nchini.

Hata hivyo hakuna muungano wa walio wengi dhidi ya ANC, kwa sababu vyama vya upinzani vya Afrika Kusini vimegawanyika sana kiitikadi.

Matokeo rasmi yanaonyesha:

• ANC ilipata 46% ya kura

• Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance (DA) 22%

• Chama cha mrengo wa kushoto cha Economic Freedom Fighters 10%

• Chama cha Zulu Inkatha Freedom Party (IFP) 6%

• Chama cha Waafrika walio wengi Freedom Front Plus 2%

• Na ActionSA kilipata 2%

Akikubali kwamba serikali za muungano zitakuwa jambo la kawaida, Rais Cyril Ramaphosa, aliyechaguliwa na ANC mwaka 2018 kusitisha kudorora kwa umaarufu wa chama hicho, alisema: "Ikiwa tunataka kufanya enzi hii kuwa mpya na bora, sisi kama viongozi lazima tuweke kando tofauti zetu."

Nini kitatokea baadaye? Wakiwa wametawaliwa na msururu wa madai ya ufisadi katika kuelekea uchaguzi wa manispaa, ANC sasa inalazimika kuwa wa kwanza kuzungumza na vyama vingine kuhusu kuunda miungano.

Mara baada ya Tume Huru ya Uchaguzi kutangaza uchaguzi, kuna dirisha la siku 14 kwa mabaraza hayo kufanya mkutano wao wa kwanza. Spika, ambaye ni lazima achaguliwe kwanza, ndipo asimamie uteuzi wa meya.

Kulingana na fujo na ghasia zilizoshuhudiwa mwaka wa 2016, mchakato huu unatarajiwa kuwa patashika na kupingwa vikali.

Uundaji wa miungano unaweza pia kuwa mgumu kutokana na kutofautiana kwa itikadi za kisiasa za vyama vinavyojadiliana.

Chanzo: BBC