Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulinzi waimarishwa Kenya kudhibiti maandamano

Ulinzi Waimarishwa Kenya Kudhibiti Maandamano Ulinzi waimarishwa Kenya kudhibiti maandamano

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Usalama umeimarishwa katika sehemu mbali mbali za Kenya huku maandamano yaliyoitishwa na upinzani kulalamikia gharama ya juu ya maisha yakiingia siku ya pili.

Katika mji mkuu Nairobi na mji wa pwani wa Mombasa ,wafanyibiashara wengi wamezifungua biashara zao kuendelea na shughuli ingawaje kwa uangalifu.

Hali mjini Kisumu -magharibi mwa nchi ni shwari huku barabara zikionekana kuwa tupu bila magari au watu wengi na maduka mengi yamesalia kufungwa.

Serikali jana ilitangaza kuwa shule zilizokuwa zimefungwa kwa siku ya kwanza ya maandamano zifunguliwe leo na masomo yaendelee.

Upinzani hata hivyo unasisitiza kwamba maandamano yataendelea licha ya kulalamikia hatua ya kukamatwa kwa viongozi wake kadhaa ambao wameripotiwa kuzuiliwa katika vitu mbali mbali vya polisi.

Mmoja wa waliokamatwa ni mbunge wa Embakasi masharikI-eneo bunge lililopo jijini Nairobi ambaye familia yake inadai amezuiliwa katika kitu kimoja cha polisi katika kaunti ya Kirinyaga,nje kidogo ya Nairobi.

Chanzo: Bbc