Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukuta wa Kanisa wauwa watoto wanne

Burundi Church Collapse Kills Ukuta wa Kanisa wauwa watoto wanne

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto wanne wamefariki dunia, baada ya ukuta wa Kanisa moja la Kipentekoste kuporomoka na kuwaangukia, huku watu wengine 15 wakijeruhiwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha eneo la kusini mwa Taifa la Burundi.

Kwa mujibu wa Afisa wa Serikali wa eneo hilo, Esperanto Inarukundo amesema Mvua hiyo kubwa iliyoandamana na upepo mkali, ilianza kunyesha eneo la Kiyange majira ya saa moja asubuhi Oktoba 15, 2023.

Amesema, ” kulikuwa na hali mbaya ya hewa na ilisababisha uharibifu mkubwa, ikiwa ni pamoja na kuporomoka kwa Kanisa la Kipentekoste la Kiyange na hao watoto walikuwa wakihudhuria madarasa ya elimu ya Dini katika Shule ya Jumapili.”

“Tunaendelea na upekuzi kwenye vifusi na tayari tumegundua miili ya watoto wanne waliokufa na majeruhi 15 Kanisani, lakini tayari Shirika la Msalaba Mwekundu la Burundi na Idara ya Ulinzi wa raia walikuwa wakisaidia shughuli ya uokoaji,” alisema Inarukundo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live