Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba amekatisha ziara yake barani Afrika kutokana na mashambulizi ya Urusi yanayoendelea nchini kwake.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twita waziri huyo amesema kwamba, toka asubuhi ya leo amekua akiwasiliana na watu wake wa karibu juu ya kinachoendelea nchini humo , na kwamba analazimika kukatisha ziara yake barani hapa na kurejea nchini Ukraine haraka iwezekanavyo.
Bw.Kuleba amekua kwenye ziara hiyo tata barani Afrika, ikiwa ni baada ya bara hili kutembelewa na Urusi kupitia kwa kiongozi wa juu wa nchi hiyo Sergei Lavrov mwezi Julai mwaka huu.
Waziri huyo tayari ameshatembelea nchi za Senegal, Ivory Coast na Ghana wakati wa ziara yake.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekua mara kwa mara akiwataka viongozi wa Afrika kulaani umavimizi wa Urusi nchini mwake.