Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukosefu wa ajira wapungua asilimia 15

3e78a93f6bf8ebd0b6b1198cebc35ad0.png Ukosefu wa ajira wapungua asilimia 15

Tue, 27 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KIWANGO cha ukosefu wa ajira nchini Rwanda kimepungua kwa asilimia 15 katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kuanzia Mei hadi Agosti mwaka huu.

Taasisi ya Taifa ya Takwimu ya Rwanda (NISR) imesema katika utafiti wake wa nguvu kazi iliyotolewa hivi karibuni kuwa, ukosefu wa ajira umepungua kutoka asilimia 22.1 ambayo ya kihistoria iliyorekodiwa Mei, mwaka huu kutokana na janga la covid-19 hadi asilimia 15 mwishoni mwa Agosti, mwaka huu.

“Hata hivyo, kiwango cha ukosefu wa ajira bado kipo juu na kinapungua taratibu kufikia asilimia 13.1 iliyokuwa Februari mwaka huu.”

“Idadi ya watu walioajiriwa imeongezeka kutoka 3,199,104 mwezi Mei mpaka 3,667,611 Agosti mwaka huu kwa ongezeko la asilimia 15, huku kukiwa na ongezeko la asilimia 6 kutoka Agosti mwaka jana mpaka Agosti mwaka huu,” alisema.

Alisema ongezeko la ajira limetokana na kufunguliwa kwa shughuli nyingi baada ya kuondolewa kwa mazuio yaliyowekwa kutokana na janga la corona ikiwamo sekta ya ujenzi kuongezeka kwa asilimia 43 na biashara asilimia 40 kwa wastani wa ongezeko la wafanyakazi 172,765.

Ajira katika sekta ya viwanda imekuwa kwa asilimia 81kwa nyongeza ya wafanyakazi 133,428, huku huduma za chakula na malazi ikiongezeka kwa asilimia 150 kwa kuwa na ongezeko la wafanyakazi 74,694

Chanzo: habarileo.co.tz