Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukata nusura uiondoe Gor Mahia Ligi ya Mabingwa

33aba513cddaa650abcf32e53d6d920e Ukata nusura uiondoe Gor Mahia Ligi ya Mabingwa

Tue, 22 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KLABU ya Gor Mahia imeliomba Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kusogeza mbele mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad uliopangwa kuchezwa kesho nchini Algeria.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Kenya wametoa ombi hilo kwa Caf baada ya kukosa usafiri wa kwenda moja kwa moja nchini Algeria kutoka Nairobi kutokana na ukata unaowakabili na kibali cha kuingia Algeria.

Gor Mahia walitarajia kusafiri juzi kwenda Algiers kwa ajili ya mchezo huo wa raundi ya kwanza wa mchujo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad lakini hadi jana ilikuwa haijasafiri. Kampuni ya Air 748 ilitoa Sh milioni 1 za Kenya kuchangia gharama za usafiri lakini tiketi zilizonunuliwa hazikutosha kwa wachezaji na maofisa waliohitajika kusafiri.

Timu hiyo inakabiliwa na ukata ambapo wachezaji wanadai kulipwa mishahara yao kabla ya kusafiri na huenda wakakosa kucheza mechi hiyo hatua ambayo itasababisha kufungiwa na kutozwa faini na CAF.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Nairobi mapema mwezi ujao na mshindi wa jumla ataingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Gor Mahia ilifuzu hatua hiyo baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa jumla ya mambao 4-3 dhidi ya APR ya Rwanda na CR Belouizdad walifuzu kwa jumla ya mabao 4-0 dhidi ya Al Nasr ya Libya. Mwenyekiti wa klabu hiyo Ambrose Rachier alikiri kuwa awali walikwama lakini wamepata suluhisho la safari yao.

“Hakuna ndege ya abiria inaruhusiwa kutua Algeria na tulilazimika kuomba idhini kutoka Algeria tumepata na tulilazimika kupewa kibali na ubalozi wao hapa Nairobi, sasa tuko huru kusafiri,” alisema Ambrose.

“Pamoja na barua ya idhini, tuliunganishwa na Shirika la Ndege la Qatar na mamlaka kwa sababu shirika hilo tu ndiyo linaruhusiwa ndani ya anga lao.” “Tunajitahidi kadiri tuwezavyo kufika Algeria, tunajaribu kupata nafasi ya kusafiri kwa pamoja tuondoke,” alisema.

Mwenyekiti huyo alieleza hatua ambazo klabu ilichukua kuhakikisha mchezo huo unachezwa. “Tulilazimika kuomba mechi kuchezwa katika nchi yoyote ya Kaskazini mwa Afrika ambapo ndege zinaruhusiwa,” aliendelea.

“Hatujapata uthibitisho wowote juu ya hilo lakini sasa tutaendelea na safari kwa sababu tumepewa idhini.”

“Kikwazo chetu kikubwa ni anga iliyofungwa ya Algeria, kutoka Nairobi ni shida.”

“Idhini ya kuingia Algeria imepatikana lakini kikwazo sasa kiko nyuma yetu,” alisema. Alisema kikwazo kingine ni kwa timu kulipa mishahara wachezaji kwani awali wachezaji wakitishia kususia mchezo huo.

Chanzo: habarileo.co.tz