Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukame waua mifugo milioni 2.6 Kenya

Ukame Ukame waua mifugo milioni 2.6 Kenya

Sat, 4 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya Mamlaka ya Taifa ya Usimamazi wa Ukame Kenya, (NDMA) idadi ya mifugo waliofariki ni asilimia 5 ya wanyama wote miliopni 52.8 katika maeneo kame na nusu kame, katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Wanayama walioathirika zaidi na kufa kwa njaa ni kondoo na ng'ombe katika kaunti mbili ambazo zimeathirika zaidi zikiwemo Marsabit na Kajiado.

Ripoti hiyo imebaini kuwa hali ya ukame imeendelea kuwa mbaya katika kaunti kame 22 kati ya 23, ikichangiwa na mvua chache katika mwaka 2022 sanjari na kukosekana kwa mvua kwa misimu minne mfululizo.

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, malisho katika maeneo kame yamekwisha kabisa kutokana na joto kali.

Hivi sasa serikali ya Kenya imetoa msaada wa shilingi bilioni 2 (sawa na dola milioni 15.68 za Kimarekani) ili kuhakikisha usambazaji wa msaada wa chakula.

Kenya ni mojawapo ya nchi katika ukanda wa Pembe ya Afrika ambayo imeathiriwa na ukame mbaya zaidi katika takriban miaka 30 iliyopita, kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu. Ripoti hiyo inasema raia milioni 5 wa Kenya wanakabiliwa na njaa. Nchi nyingine mbili zilizoathirika katika Pembe ya Afrika ni Somalia na Ethiopia.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Somalia inashuhudia miaka mitano ya uhaba wa mvua, hali ambayo haijaonekana katika miaka zaidi ya 40 iliyopita, na msimu wa sita wa uhaba wa mvua unatarajiwa kuzifanya familia zaidi kukimbia makazi yao.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, maeneo ya kusini na mashariki mwa Ethiopia yanakabiliwa na athari mbaya za ukame na kuna haja ya kuchukuliwa hatua za haraka kukabiliana na hali hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live