Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukame watawala maradufu Pembe ya Afrika

Njaa 1 (600 X 398) Ukame watawala maradufu Pembe ya Afrika

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenendo wa ukame katika Pembe ya Afrika unaripotiwa kuwa mbaya zaidi hivi sasa kuliko ilivyokuwa wakati wa njaa ya 2011 ambapo mamia ya maelfu ya watu waliaga dunia.

Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa cha Jumuiya ya IGAD jana kilieleza kuwa, mvua za chini ya kiwango cha kawaida zinatazamiwa kunyesha miezi mitatu ijayo. Taarifa ya kituo hicho imebainisha kuwa, hii inaweza kuwa msimu wa mvua uliofeli mara sita mtawalia katika maeneo ya Ethiopia, Kenya, Somalia na Uganda ambayo yameathirika pakubwa na ukame wa sasa. Si hayo tu, bali hali ya kukosekana mvua kusiko kwa kawaida imeripotiwa kuongezeka katika baadhi ya maeneo ya Burundi, mashariki mwa Tanzania, Rwanda na magharibi mwa Sudan Kusini. Ukame na athari zake katika eneo la Pembe ya Afrika

Wakati huo huo Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa jana alisema kuwa watu milioni 8.3 ambao ni zaidi ya nusu ya jamii ya wananchi wa Somalia watahitaji misaada ya kibinadamu mwaka huu. Workneh Gebeyehu Mkuu wa Jumuiya ya IGAD amezihimiza serikali za nchi zilizoathiriwa na ukame na washirika wao kuchukua hatua haraka iwezekanavyo.

Hali ya ukame ambayo imedumu kwa muda mrefu huko Somalia yaani kwa karibu miaka mitatu sasa umesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya watu. Ukame, ambao ni mrefu zaidi kuwahi kurekodiwa nchini Somalia, umedumu kwa takriban miaka mitatu na makumi ya maelfu ya watu wamekufa.

Mwezi uliopita Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia alitahadharisha kuwa bila shaka vifo zaidi nchini humo vitapindukia idadi ya watu waliopoteza maisha wakati njaa ilipoiathiri nchi hiyo mwaka 2011; ambapo watu zaidi ya 260,000 waliaga dunia kwa kukosa chakula.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live