Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukame Somalia kuwaacha watu milioni 1.4 bila makazi

Drought Somali Ukame Somalia kuwaacha watu milioni 1.4 bila makazi

Fri, 28 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha huku mamilioni wakikadiriwa kukosa makazi endapo hatua za haraka hazitachukuliwa kudhibiti madhara ya ukame ambao umeikumba nchi ya Somalia kwa muda mrefu sasa.

Hadi sasa jumla ya watu 245,000 nchini humo wameripotiwa kukosa makazi kufuatia janga hilo hata hivyo idadi hiyo inatarajiwa kupanda zaidi hadi kufika watu milioni 1.4 mwaka 2022.

Ukame huo unatajwa kuathiri watu karibu milioni 3.2 hadi sasa sawa na asilimia 50 ya idadi ya watu wote nchini humo na kuacha watu hao wakiwa kwenye ugumu wa kupata huduma za msingi kama vile maji na chakula jambo ambalo limepelekea kupanda kwa gharama za bidhaa, utapia mlo, vifo vya mifugo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live