Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujerumani kurudisha sanamu takatifu iliyoibiwa Cameroon

Camerron Ujeruman Ujerumani kurudisha sanamu takatifu iliyoibiwa Cameroon

Wed, 29 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ujerumani imekubali kurudisha sanamu takatifu iliyoibwa kutoka Cameroon mwanzoni mwa karne iliyopita.

Wakfu wa Urithi wa Utamaduni wa Prussian, ambao unasimamia makumbusho ya mji mkuu wa Ujerumani, ulisema utamrejesha mtu wa kike, anayejulikana kama Ngonnso, kwa jamii ya Nso kaskazini-magharibi mwa Cameroon.

Sanamu hiyo ilichukuliwa na afisa wa kikoloni na kukabidhiwa kwa Jumba la Makumbusho la Ethnological la Berlin mwaka wa 1903.

Mwana wa mfalme wa Nso aliambia shirika la habari la Reuters kwamba habari hizo zilipokelewa kwa furaha nchini Cameroon.

‘’Baada ya zaidi ya miaka 120, tunaweza tu kubaki na furaha kwa kuwa ni wakati wa kuadhimisha na kuwa karibu na uhusiano wa mababu zetu kwa upendo na umoja,’’ Mbinglo Gilles Yumo Nyuydzewira alinukuliwa akisema.

Taasisi hiyo pia ilisema kwamba itarudisha vipande 23 Namibia na inapanga makubaliano ya kurejesha vitu nchini Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live