Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi uwanja wa ndege Kabaale wafikia asilimia 55

5f3e7cfd627d378b36567e5378d25ef8.jpeg Ujenzi uwanja wa ndege Kabaale wafikia asilimia 55

Fri, 4 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

UJENZI wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kabaale kilichopo Kaunti ya Buseruka wilayani Hoima, umefikia asilimia 55.

Hayo yamebainishwa na Mamlaka ya Petroli Uganda (PAU).

Meneja Uhusiano kwa Umma wa PAU, Gloria Ssebikari, alisema ujenzi wa kiwanja hicho ulianza mwaka 2018 baada ya Kampuni ya SBC Uganda ambayo ni Kampuni tanzu kati ya Kampuni ya Colas ya Uingereza na Kampuni Kimataifa ya SBI Holdings ya Uganda kuruhusiwa na Serikali ya Uganda.

“Katika kutekeleza mradi huo ikiwemo ujenzi wa mifereji ya maji na njia ya kurukia ndege yenye urefu wa kilometa 3.5 inakaribia kukamilika ambapo mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 55,”alisema Ssebikari.

Alisema kukamilika kwa ujenzi wa kiwanja hicho cha pili cha kimataifa ni sehemu ya miradi kadhaa ya mafuta ambayo wakazi wa Hoima na Uganda kwa ujumla watanufaika nayo.

“Tunaendelea vizuri. Tunatarajia maeneo jirani na mradi huo kukua ili Hoima ije kuwa jiji kubwa. Mradi huu unaogharimu Dola bilioni 3.5 unatarajiwa kukamilika mwezi Februari 2023,” alisema Ssebikari.

Ssebikari aliongeza kuwa mkazo mkubwa kwa sasa pia umeelekezwa kwenye ujenzi wa jengo la kisasa kiwanjani hapo kwa ajili ya kuhudumia abiria na mizigo, mifumo ya umeme, kituo cha zimamoto, maegesho ya magari, barabara za kuingia na kutoka na mnara wa kuongozea ndege

Chanzo: www.habarileo.co.tz