Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi soko la Afrika Mashariki mbioni kuanza

71d1e982cd23e5a4fce6aa992df94a17.png Ujenzi soko la Afrika Mashariki mbioni kuanza

Tue, 10 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

UJENZI wa soko la ukanda wa Afrika Mashariki katika mpaka wa Tanzania na Uganda, Mutukula wilayani Kyotera unatarajiwa kuanza Desemba mwaka huu.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Rural United Business Association Network (RUSBA) Ltd, Karim Karamagi alisema hivi karibuni kuwa soko hilo la kikanda litajengwa katika kijiji cha Kasanvu kwenye barabara ya Kyotera- Mutukula.

Ujenzi huo uliosubiriwa kwa muda mrefu umehamasishwa na wafanyabiashara na viongozi wa maeneo hayo.

Ujenzi wa soko hilo unaofadhiliwa na Kampuni ya Afrika Kusini ya Degitech Energy Company Ltd utagharimu Sh trilioni 2.8 za Uganda.

Litakapokamika linatarajiwa kuwakutanisha wenye viwanda, wauzaji wa jumla, wasambazaji na wateja kutoka nchi za EAC.

Karamagi alisema wamepata baadhi ya fedha na kuamua kuanza ujenzi kwa kuwa walitarajia ujenzi huo ungeanza mapema zaidi lakini kutokana na maambukizi ya virusi vya corona umechelewa.

“Ilibidi kusubiri kidogo na sasa tumepata fedha na mazuio yaliyowekwa kutokana na mlipuko wa corona yameondolewa kwa kiasi kikubwa, hivyo tumeamua kuanza kazi ya ujenzi,” alisema Karamagi.

Soko hilo litakuwa likifanya kazi siku za Jumanne na Ijumaa na pia litakuwa na uwanja wa kuhifadhi wanyama wakiwamo kondoo, mbuzi na ng'ombe. Mifugo hiyo itahifadhiwa kwa muda kwa ajili ya kuchinjwa na kuuza nyama kwenye masoko ya ndani na ya kimataifa.

Karamagi alisema walipata ekari 200 za ardhi walizokodisha kutoka serikali ya mtaa huo na kwamba soko hilo litakuwa na miundombinu yote.

Mutukula iko Kusini mwa wilaya ya Kyotera katika mpaka wa kimataifa kati ya Uganda na Tanzania takriban kilometa 225.1 kwa barabara kutoka Kampala.

Mwaka 2017, mpaka wa Mutukula ulikuwa kituo cha pamoja kikifanya kazi saa 24 za usafirishaji wa bidhaa, abiria na mauzo ya nje yanayopita mpaka huo kwenda Tanzania na Uganda.

Katibu Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Kagera, Rwechungura Mali amesema ujenzi wa soko hilo ni fursa kubwa kwa Watanzania kwani asilimia 70 ya chakula kwa nchi za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wanategemea Tanzania.

Chanzo: habarileo.co.tz