Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi barabara kuu ya Nairobi wafikia asilimia 33

E346e1cb21570c684a7caafffa8a071a Ujenzi barabara kuu ya Nairobi wafikia asilimia 33

Tue, 6 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI wa Uchukuzi, James Masharia amesema ujenzi wa barabara kuu ya Nairobi Expressway inayogharimu Sh bilioni 60 umefikia asilimia 33.

Macharia ambaye alikuwa katika ziara ya ukaguzi wa barabara hiyo hivi karibuni, alisema mradi huo unaendelea vizuri na kueleza kuwa na imani utakuwa tayari kutumika mwishoni mwa mwaka huu.

Barabara hiyo ya kilometa 27.1 inayoanzia Mlolongo kupitia barabara kuu ya Uhuru, awali ujenzi wake ulikadiriwa kuchukua miaka miwili baada ya kuzinduliwa na Rais Uhuru Kenyatta Oktoba 2019 na ilitarajiwa kukamilika na kufunguliwa mapema mwaka ujao.

Macharia alisema barabara hiyo ni kiungo muhimu katika ukanda wa Kaskazini ambao ndio lango kuu la usafirishaji na uagizaji bidhaa kwenda na kutoka Bandari ya Mombasa kuelekea nchi jirani za Uganda, Rwanda, Burundi na Kusini na Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Alisema barabara hiyo itakuwa ikibeba asilimia 85 ya mizigo na abiria katika maeneo ya Athi River, Kitengela, Mlolongo, Syokimau, Utawala, Embakasi, Kusini B na Kusini C na maeneo ya karibu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz