Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uingizaji wa bidhaa za Uganda washuka

174240cbf471ab484a7ea780263a9530 Uingizaji wa bidhaa za Uganda washuka

Tue, 20 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

NAIROBI

UINGIZAJI wa bidhaa nchini kutoka Uganda umeshuka kwa mwezi Agosti kutokana na kuchelewa kwa mizigo mpakani na kufanya shughuli za uchumi kushuka sababu ya mlipuko wa virusi vya corona.

Bidhaa za Uganda zinazoingia Kenya zina thamani ya dola za Marekani milioni 46.9 sawa na Sh bilioni 5.1 za Kenya kwa Agosti ikiwa imeshuka kutoka Sh bilioni 5.2 katika kipindi kama hicho mwaka uliotangulia.

Taasisi ya Takwimu Uganda imesema kiasi cha bidhaa za Kenya zilizoingia Uganda kimeongezeka kwa Sh bilioni 9.6, ikiwa ni ongezeko kutoka Sh bilioni 5.9 katika kipindi hicho mwaka jana, huku kuchelewa kwa mizigo katika mipaka ya Malaba na Busia kukiendelea kuathiri biashara hizo.

Kenya imekuwa ikiingiza bidhaa kutoka Uganda za aina ya maziwa, tumbaku, miwa, nishati ya umeme na nyinginezo, huku yenyewe ikiuza mafuta ya kupikia, chumvi na bidhaa nyingine ikiwamo za bati na chuma.

Uganda imeendelea kuwa mshirika mkubwa wa biashara na Kenya katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa asilimia 28 ya bidhaa zinazosafirishwa Afrika, huku uuzaji wa bidhaa katika soko la Afrika Mashariki ukiongezeka kwa asilimia nane kufikia Sh bilioni 140.4.

Chanzo: habarileo.co.tz