Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uingereza yapiga marufuku za safari Kenya

45087 Pic+kenyata Pigo jingine la Utalii Kenya:

Sat, 28 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wasafiri kutoka Kenya bado wamesalia na marufuku yakuingia Uingereza kufuatia hatua ya hivi karibuni iliyochukuliwa na Uingereza siku ya alhamis jioni jambo ambalo linatajwa kuathiri upya msimu huu wa Utalii nchini Kenya.

Uingereza ilitoa orodha ya mataifa yaliyopo kwenye kile walichokiita "Red List" Kenya ikiwemo, kutokana na wasiwasi juu ya kuenea kwa virusi vipya vya Corona vilivyoripotiwa nchini Kenya.

Awali Uingereza iliiweka Kenya kwenye orodha hiyo mwezi Aprili, kutokana na takwimu za maambukizi zinazoendelea kuongezeka muda wa marufuku wa kusafiri umeongezwa maradufu.

Uamuzi huo ni pigo jingine kwa Kenya katika sekta ya utalii kwani msimu wa kupokea wageni Kenya huanza mwezi July na kumalizika mwezi Septemba ambao huenda sambamba na msimu wa kiangazi wa nchi hiyo unaombatana na uhamaji mashuhuri wa nyumbu na pundamilia katika Pori la hifadhi la Maasai Mara.

Kenya ni kitovu maarufu cha Utalii kwa uingereza. Na Uingereza ni moja ya soko kubwa la utalii Kenya. Mwaka 2019 ilishika nafasi ya nne kwa idadi ya watalii 181,484 kutoka Uingereza.

Uingereza imeyagawa mataifa yaliyowekewa vikwazo kuingia Uingereza kwa rangi ambapo baadhi zimepewa rangi ya kijani, kijani kibichi na Nyukundu na masharti tofauti ili kupunguza kuneo kwa virusi vya Corona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live