Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uingereza yang'ang'ania kupeleka wakimbizi Rwanda

Rwandaaaaaaaaa Uingereza Wakataa Uingereza yang'ang'ania kupeleka wakimbizi Rwanda

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, amesema amejitolea kuhakikisha mpango wa serikali yake wa kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda, unatekelezeka, baada ya mahakama ya juu wiki iliyopita kuamua kuwa ni mpango huo ni kinyume cha sheria.

Sunak ameahidi kuanzisha mkataba mpya na sheria ya dharura ili kufanikisha hilo licha ya kuwepo ripoti kuwa baraza lake la mawaziri limegawanyika.

Aidha amesema wamekuwa wakifanyia kazi mkataba mpya na Rwanda ambao utashughulikia maswala yote yaliyoibuliwa na Mahakama ya Juu, na kulipa bunge nafasi ya kuthibitisha kwamba Rwanda ni mahali salama pa kutekeleza mpango huo.

Waziri wa uhamiaji Robert Jenrick, anashinikiza sheria hiyo kutozingatia haki za kibinadamu na kuelekeza mahakama kupuuza mkataba wa Ulaya wa haki za kibinadamu kuhusu wakimbizi, hata hivyo amekabiliwa na ukosolewaji mkubwa.

Utawala wa Kigali unasema kuwa nchi yake ni salama kwa waomba hifadhi hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live