Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uingereza yang'ang'ania kupeleka wakimbizi Rwanda

Rwandaaaaaaaaa Uingereza Wakataa Uingereza yang'ang'ania kupeleka wakimbizi Rwanda

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Uingereza imesema itaingia makubaliano mapya na Rwanda kwa ajili ya kufufua mpango wake wa kuhamishia waomba hifadhi nchini humo, licha ya hukumu ya mahakama ya juu kusema mpango huo ni kinyume cha sheria.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo kali iliyotikisa serikali yake, Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ambaye aliahidi kuzuia wahamiaji wanaowasili Uingereza katika boti ndogo ndogo kupitia njia ya bahari ya English Channel, amesema hukumu hiyo haikuwa na matokeo aliyoyataka huku akiapa kuendelea na mpango wake wa safari za kwanza za ndege za wahamiaji kwenda Rwanda msimu ujao wa machipuko.

Alisema mahakama ilithibitisha kuwa kanuni ya kuwahamisha waomba hifadhi katika nchi nyingine iliyo salama ni halali, licha ya kuhitimisha kwamba Rwanda haiko salama. Waziri Mkuu Sunak ameahidi kupitisha sheria bungeni, itakayohakikisha kuwa Rwanda itakuwa salama, na kuhakikisha mpango wake hauzuwiliwi na mahakama za kigeni.

Mahakama ya Juu ya Uingereza imesema mpango wa serikali ya London wa kuwapeleka nchini Rwanda wakimbizi na waomba hifadhi walioko nchini humo unakiuka sheria. Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak

Mahakama hiyo ilitoa uamuzi huo siku ya Jumatano ikisisitiza kuwa, mpango huo unawaweka katika hali hatarishi wakimbizi hao, hasa kwa kuzingatia kuwa baadhi yao waliikimbia nchi yao ya Rwanda na kuwarejesha huko ni kuwaweka hatarini.

Uamuzi wa umekuja baada ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza kuwasilisha rufaa kupinga uamuzi wa awali wa Mahakama ya Rufaa iliyosema pia kuwa mpango wa kuwatuma waomba hifadhi nchini Rwanda ni kinyume cha sheria.

Mpango huo wa serikali ya Uingereza umekuwa ukipingwa vikali na mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu, wanaosema Rwanda haiwezi kuwa nchi salama kwa wakimbizi na wahamiaji hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live