Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uingereza yakaliwa kooni sakata la wahamiaji Rwanda

Rwanda Yawapokea Makumi Ya Wakimbizi Kutoka Libya Uingereza yakaliwa kooni sakata la wahamiaji Rwanda

Tue, 23 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya kutetea haki za binadamu barani Ulaya, imetoa wito kwa Uingereza kutupilia mbali mpango wake wenye utata wa kuwatuma waomba hifadhi nchini Rwanda, wito unaokuja baada ya bunge jijini London kupitisha mswada huo.

Kwa mujibu wa kamishena wa tume hiyo barani Ulaya Michael O'Flaherty, mpango huo kati ya serikali ya Kigali na ile ya Uingereza, unaibua maswali mengi kuhusu haki za waomba hifadhi na sheria kwa ujumla.

Bunge nchini Uingereza siku ya Jumatatu lilipitisha mswada unaoruhusu kutumwa kwa waomba hifadhi nchini Rwanda wakati wakisubiri uamuzi kuhusu maombi lao.

O'Flaherty pia alionya kuwa mswada huo unazuia kwa kiasi kikubwa mahakama za Uingereza kuangazia kikamilifu na kwa uhuru maswala yanayowasilishwa mahakamani.

Mpango huo ambao umekashifiwa na wataalam wa masuala ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa na makundi yanayotetea haki za waomba hifadhi, umekabiliwa na changamoto za kisheria tangu ulipopendekezwa mwaka wa 2022.

Serikali ya Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak imekuwa ikikabiliwa na shinikizo la kukabiliana na idadi kubwa ya waomba hifadhi wanaoingia nchini humo wakitokea kaskazini mwa Ufaransa kwa kutumia boti ndogo.

Umoja wa Mataifa pia umetoa wito kwa Uingereza kuangazia upya mpango huo ikisema kuwa ni tishio kwa utawala wa sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live