Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uingereza yafuta safari ya kwanza ya ndege kuhamisha wakimbizi Rwanda

Wakimbizi Rwanda Uingereza yafuta safari ya kwanza ya ndege kuhamisha wakimbizi Rwanda

Wed, 15 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Safari ya kwanza ya ndege ambayo ilikusudiwa na Uingereza kuwasafirisha kwa lazima wakimbizi na kuwapeleka nchini Rwanda, imeahirishwa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, safari hiyo ya ndege kutoka Uingereza kuelekea Rwanda iliakihirishwa dakika za mwisho jana Jumanne, baada ya Bunge la Haki za Binadamu la Ulaya kutoa amri ya kusimamishwa zoezi hilo.

Kabla ya hapo na baada ya serikali ya Uingereza kutangaza kuwa kundi la kwanza la wakimbizi waliokimbilia nchini humo lilipandiwa kupelekwa Rwanda jana Jumanne, jana hiyo hiyo serikali ya Kigali ilisema kuwa, imejiandaa vizuri kuwapokea na kuwahudumia wakimbizi hao.

Hatua hiyo imekuja baada ya mahakama ya rufaa ya mjini London kuidhinisha juzi Jumatatu uamuzi wa mahakama ya chini ambayo ilitupilia mbali ombi la kutaka kusimamishwa mpango wa kuwapeleka wakimbizi hao nchini Rwanda.

Msemaji wa serikali ya Rwanda, Bi Yolande Makolo amewaambia waandishi wa habari kuwa, wakimbizi wote watakaopelekwa nchini humo kutoka Uingereza watapewa huduma zote zikiwemo za kisheria na kurahisishwa kubakia nchini humo hadi masuala yao ya ukimbizi yatakapokamilika.

Ijapokuwa Makolo hakusema idadi hasa ya wakimbizi hao watakaopelekwa Rwanda kutokea Uingereza, lakini amesema kuwa Kigali iko tayari kupokea maelfu ya wakimbizi hao.

Msemaji huyo wa serikali ya Rwanda pia amesema, wakimbizi hao watakuwa huru kuingia nchini humo wakati wowote wanaopenda na wakati wowote watakapoamua kuondoka Rwanda na kurejesha katika nchi zao au katika nchi yoyote itakayokubali kuwapokea, pia watakuwa huru kufanya hivyo. Lakini amesema, iwapo maombi ya ukimbizi yatakataliwa ndani ya Rwanda, wakimbizi hao watakuwa huru kuomba hata uraia wa nchi hiyo ndogo ya katikati mwa Afrika.

Kabla ya hapo pia, Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR Filippo Grandi, naye alikuwa amekosoa uamuzi wa serikali ya Uingereza wa kuwahamishia Rwanda watafuta hifadhi wanaokimbilia nchini humo huku akisema makubaliano hayo ya kando kati ya nchi mbili hizo ni makosa.

Makubaliano hayo yamefikiwa baina ya serikali za Kigali na London baada ya Uingereza kushindwa kufikia makubaliano kama hayo na nchi za Kenya, Ghana na Albania. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, serikali ya Rwanda itapewa dola milioni 158 na serikali ya Uingereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live