Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uingereza: Rwanda ni salama kwa wakimbizi

Rwanda Wakimbizi Ndege Uingereza: Rwanda ni salama kwa wakimbizi

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

OFISI ya Mambo ya Ndani ya Uingereza imesisitiza kuwa Rwanda ni mahali salama kwa wakimbizi ambao wanaweza kuhamishiwa huko chini ya mpango wa nchi yake wa pauni milioni 140 (Sh bilioni 397.8) wa kuondoa wahamiaji hao.

Katibu wa Ofisi hiyo, Suella Braverman alitoa kauli hiyo wakati wa ziara ya kikazi nchini Rwanda wiki hii, na kuthibitisha "kujitolea kwa Uingereza ni ushirikiano wa msingi," ambao ni kama "kizuizi muhimu dhidi ya safari hatari na haramu" zinazofanywa na wahamiaji.

Alizuru katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali kushuhudia nyumba ya kisasa inayojengwa kwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji watakaoondolewa Uingereza na pia kupanua mpango wa kuwahamisha wahamiaji wote wanaoingia kinyume cha sheria katika ardhi ya Uingereza baada ya kupita katika nchi ‘salama’.

Ingawa makubaliano kati ya mataifa hayo mawili, ambayo yametengana takriban kilomita 6,500, yamekuwepo tangu mwaka jana, hakuna (mkimbizi) aliyehamishiwa katika taifa hilo la katikati mwa Afrika, kutokana na masuala ya kisheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live