Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhusiano Tunisia, Syria wazidi kupamba moto

Tunisia Syria Uhusiano Tunisia, Syria wazidi kupamba moto

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Balozi mpya wa Syria nchini Tunisia, Mohamed Mohamed, jana Jumatatu alikabidhi hati zake za utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia, Nabil Ammar, ikiwa ni ishara ya kuzidi kuimarika uhusiano wa nchi hizo mbili.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Tunisia imesema kuwa, katika mazungumzo baina ya balozi mpya wa Syria na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia mjini Tunis, pande hizo mbili zimetilia mkazo wajibu wa kuendelezwa uhusiano wa kihistoria kati ya nchi hizo mbili ndugu za Kiislamu na kuahidi kuimarisha zaidi ushirikiano wa pande mbili katika nyanja zote.

Tarehe 27 Aprili, Rais Kais Saied wa Tunisia alimteua Mohamed Mhadhbi kuwa balozi mpya wa nchi hiyo nchini Syria, wakati nchi hizo mbili zilipoingia kwenye mkono wa kurejesha uhusiano wa kidiplomasia ambao ulikatishwa mwezi Februari 2012, takriban mwaka mmoja baada ya kuzuka Syria kutumbukizwa kwenye vita na magenge ya kigaidi yaliyomiminwa nchini humo na maadui kutoka kona zote za dunia.

Tunisia ilitangaza rasmi kuteua balozi balozi wake wa kuiwakilisha nchi hiyo huko Syria baada ya kufikiwa uamuzi wa wa pamoja wa nchi hizo mbili wa kurejesha uhusiano wao wa kidiplomasia kikamilifu.

Balozi mpya wa Tunisia nchini Syria ambayo ni mwanadiplomasia mwandamizi, Mohamed Mhadhbi, alipewa hati zake za utambulisho na Rais Kais Saied wakati wa hafla iliyofanyika kwenye Ikulu ya Carthage jijini Tunis mwezi huo wa Aprili.

Wakati wa hafla hiyo, Mohamed Mhadhbi, balozi mpya wa Tunisia nchini Syria alisema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa nitafanya kila niwezalo kwa dhati na kwa moyo wote kutekeleza wajibu mtakatifu wa taifa kwa namna bora kabisa pamoja na majukumu ya kiongozi mkuu kwa maslahi ya nchi na kwa kuhheshimu katiba na sheria za wa nchi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live