Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhuru atua Zambia kuhudhuria mazishi ya Rais mstaafu Kenneth Kaunda

Uhuru Kenyata?fit=800%2C445 Uhuru atua Zambia kuhudhuria mazishi ya Rais mstaafu Kenneth Kaunda

Sat, 3 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Rais Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa viongozi wa mataifa ya Barani Afrika ambao wanatarajiwa kuhudhuria hafla ya mazishi ya mwendazake Rais mstaafu wa Zambia Kenneth Kaunda.

Kaunda ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa nchi hiyo, alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa Nimonia akiwa na umri wa miaka 97.

Mwili wake umekuwa ukizungushwa katika mikoa ya nchi hiyo na wanajeshi ili wananchi wapate fursa ya kumpa heshima zake za mwisho.

Uhuru aliandamana na afisa mkuu katika ikulu ya Nairobi Nzioka Waita ambaye aliwataarifu mashabiki wake mitandaoni kwamba alikuwa ametua mjini Lusaka na Rais.

Kama ilivyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, Uhuru alikamilisha ziara yake nchini Ufaransa Julai 2 kabla ya kutua Zambia.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramahosa pia ametua nchini Zambia kwa ajili ya kuhudhuria hafla hiyo.

Ramaphosa alimteua Waziri wa Elimu Angie Motshekga kuhudumu kama kaimu Rais kwa siku chache ambazo hatakuwa nchini humo

Hii ni kwa sababu naibu wake David Mabuza amelazwa katika hospitali moja nchini Russia ambapo anapokea matibabu.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke