Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhuru amuidhinisha Raila kuwa mrithi wake akiwa ziarani Kibera

B6b7bacc9c0ba0be Uhuru amuidhinisha Raila kuwa mrithi wake akiwa ziarani Kibera

Thu, 30 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Rais Uhuru Kenyatta amemuidhinisha Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kuwa mrithi wake atakapostaafu mwaka wa 2022.

Akiwahutubia wakazi wa mtaa wa Kibera Jumanne, Septemba 29, Uhuru alionekana kuashiria kwamba Raila ndiye mwanasiasa bora zaidi kuendeleza miradi yake ya maendeleo na kudumisha amani nchini.

Uhuru ambaye alikuwa ameandamana na Raila kwenye hafla hiyo, aliwaambia wakazi wafanyae uamuzi ufaao ambao hawatajutia baada ya uchaguzi mkuu wa 2022.

"Niwaulize, si tumekuwa na amani nchini tangu tulipoafikiana kufanya kazi kwa pamoja? si tumeona maendeleo makubwa baada ya salamu za amani? Mnataka kazi iendelee? uamuzi ni wenu sasa."

"Mtafanya maamuzi yafaayo? katika uchaguzi mkuu wa 2022? Haya basi kazi kwenu." Uhuru alisema huku akishangiliwa na umati.

Awali Uhuru alikuwa amekana kwamba hajampata mwanasiasa bora ambaye angemuidhinisha kumuunga mkono ingawa amekuwa akionyesha dalili ya kumvulia koti waziri huyo mkuu wa zamani.

Wachanganuzi wa masuala ya kisias wamekuwa wakichanganua kwamba Raila anatayarishwa kuliongoza taifa ikizingatia tofauti zilioko kati ya Rais na Naibu wake William Ruto.

Hatua ya Uhuru kumuidhinisha Raila inajiri siku chache baada ya kinara huyo wa ODM kukutana na wafanyabiashara tajika kutoka eneo la Mlima Kenya ambao wengi wao wametangaza kumuunga mkono 2022.

Kwenye mkutano uliofanyika mjini Nairobi Jumanne Septemba 28,viongozi wa chama cha Mount Kenya Foundation(MKF) walisema Uhuru alikuwa amewapa jukumu la kutambua mwanasiasa bora ambaye atamrithi.

" Rais alitupa jukumu la kumsaidia kutafuta mwanasiasa ambaye atamurithi mwaka wa 2022, alitaka tumshauri ni mwanasiasa wa aina gaina atakuwa bora," Naibu mwenyekiti wa chama hicho Titus Ibui alisema.

Aidha, chama hicho pia kilisema kwamba kitafanya mkutano na vinara wa muungano wa OKA ili kutafuta mrithi wa Uhuru.

" Tukishamaliza kufanya mikutano yetu, tutaketi chini tujadiliane na tumchague ule mgombea bora ba tuwasilishe majina yake kwa Rais." Aliongezea Ibui

Wanasiasa wamekuwa wakimshinikiza Uhuru ametaja mrithi wake tangu Naibu Wake alipokiunda chama kipya cha UDA.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke