Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhuru amsimamisha kazi jaji wa Mahakama Kuu baada ya udhaifu wa akili

0fgjhs3004l2q4b7p Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Wed, 25 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Rais Uhuru Kenyatta amemsimamisha kazi Jaji wa Mahakama ya Ardhi Muthoni Gathumbi kutokana na kutokuwa na uwezo unaofaa kiakili kutekeleza majukumu yake.

Jaji wa Mahakama ya Ardhi Muthoni Gathumbi amemsimamishwa kazi kutokana na kutokuwa na uwezo unaofaa kiakili kutekeleza majukumu yakeHii ni kufuatia ushauri wa Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) kwa rais Uhuru.

Rais Uhuru alisema JSC ilimueleza kuwa jaji huyo hawezi kutekeleza majukumu yake ifaavyo

Hii ni kufuatia ushauri wa Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) baada ya kuteua jopo la kuchunguza ufaafu wa Jaji Gathumbi kuhudumu.

Akitoa uamuzi wake uliochapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali Jumanne, Agosti 24, Rais Uhuru alisema JSC ilimueleza kuwa jaji huyo hawezi kutekeleza majukumu yake ifaavyo.

"JSC, baada ya kuchunguza ripoti kadhaa za matibabu, iliridhika na sababu za kumuondoa Jaji Githumi ofisini kutokana na kukosa uwezo wa kutekeleza majukumu yake zilizokuwa zimethibitishwa chini ya kipengee cha 168 (1) (a) cha katiba," ilisoma notisi hiyo.



Jaji Gathumbi alikuwa akihudumu katika kitengo cha kusikiliza kesi za mizozo ardhi.

Uteuzi wa jopoKisheria, Rais huteua jopo la kuchunguza madai kama hiyo kutoka kwa JSC na kisha kuwasilisha ripoti kwake.

Kufuatia ombi hilo la JSC, Uhuru ameteua jopo litakalochunguza na kuthibitisha madai ya kumuondoa Jaji Gathumbi ofisini likiongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu Omondi Hellen Amolo.

Wanachama wengine ni majaji Luka Kiprotich Kimaru, Linnet Ndolo, Peter Munge Murage na Mary Martha Nyakado Bonyo.

Ripoti ya jopo hilo ndio itaamua iwapo Rais Kenyatta atakubali ombi la JSC la kumuondoa Jaji Gathumbi ofisini.

Iwapo jopo hilo litashindwa kuthibitisha madai ya JSC, basi Jaji Gathumbi ataendelea kuhudumu.

Hii ni mara ya kwanza JSC kupendekeza jaji kuondolewa ofisini kwa madai ya udhaifu wa akili.

Jimmy Wanjigi Atua Nakuru kwa Kishindo, Asema Yuko Tayari kwa 2022

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke