Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhuru, Raila wamuomboleza Desmond Tutu, wasema Afrika imepoteza shujaa wa amani

C69231947e049002 Uhuru, Raila wamuomboleza Desmond Tutu

Sun, 26 Dec 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Rais Uhuru Kenyatta alimuomboleza marehemu, Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Desmond Tutu, aliyeaga dunia Jumapili, Desemba 26 akiwa na umri wa miaka 90

Alisema si tu kwamba ni Afrika Kusini pekee iliyopata pigo bali Afrika nzima kwa ujumla inaomboleza shujaa wa uhuru, amani, na maridhianoKiongozi wa ODM kwa upande wake alisema Afrika imepoteza shujaa wa ukombozi Desmond Tutu Rais Uhuru Kenyatta ameungana na viongozi wa dunia kuomboleza kiongozi wa Afrika Kusini aliyepinga ubaguzi wa rangi na Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Desmond Tutu, aliyefariki dunia Jumapili, Desemba 26 akiwa na umri wa miaka 90.

Katika rambirambi zake, Uhuru alimuomboleza Askofu Mkuu Desmond Tutu kama mwanasiasa wa Afrika wa uhuru, amani na maridhiano, akisema kuwa kifo chake ni pigo kubwa kwa Afrika Kusini na Afrika, ambako kasisi huyo anaadhimishwa kama mtetezi wa amani.

"Kuaga dunia kwa Askofu Mkuu Desmond Tutu ni pigo kubwa sio tu kwa Jamhuri ya Afrika Kusini ambapo ameacha nyayo kubwa kama shujaa wa kupinga ubaguzi wa rangi lakini kwa bara zima la Afrika ambako anaheshimiwa na kama mpenda amani," alisema kiongozi wa taifa.

Read also

Askofu Maarufu wa Afrika Kusini Desmond Tutu Aaga Dunia

Kupitia mafundisho ya Tutu, Uhuru alisema kuwa kizazi kipya cha viongozi wa Afrika waliepukana na vurugu katika harakati zao za kupigania uhuru.

"Kupitia kazi yake iliyotukuka kwa miaka mingi kama kasisi, mpigania uhuru na mtunza amani, Askofu Mkuu Tutu alihamasisha kizazi cha viongozi wa Afrika ambao walikubali mbinu zake zisizo za vurugu katika mapambano ya ukombozi," Uhuru alisema kuhusu mkuu wa zamani wa Kanisa la Anglikana la Afrika Kusini.

Aliyekuwa waziri mkuu Raila Odingakwa upande wake alisema Afrika imepoteza shujaa wa ukombozi Desmond Tutu.

"Bara limepoteza kiongozi mwenye sifa na ushujaa mkubwa. Nitathamini wakati niliopata fursa ya kubadilishana mawazo juu ya mustakabali wa bara letu, bara ambalo alifanya mengi kuinua machoni pa ulimwengu mzima," Waziri Mkuu huyo wa zamani alisema.

Raila aliangazia zaidi jukumu la Tutu katika kujaribu kutatua mgogoro wa baada ya uchaguzi wa 2007/2008 nchini Kenya, akisema alikuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza kujaribu kuzima machafuko hayo.

"Kwetu sisi, Tutu alikuja hapa kama mtalii ... kwa sababu hatukumwalika kuzungumza nasi," afisa mkuu wa serikali aliambia wanahabari.

Askofu Mkuu Desmond Mpilo Tutu alikuwa mhubiri wa muda mrefu wa Kanisa la Anglikana na mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi ambaye alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 1984.

Tutu baadaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Tume ya Ukweli na Maridhiano ya Afrika Kusini baada ya ubaguzi wa rangi.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke