Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhaba wa vifaa vya ndege wasababisha Kenya Airways kusuasua

Marubani Wanaogoma Kenya Kuchukuliwa Hatua Uhaba wa vifaa vya ndege wasababisha Kenya Airways kusuasua

Tue, 10 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la ndege la Kenya Airways linasema kuwa linakabiliwa na changamoto katika usafiri wake kutokana na kuchelewa kupata baadhi ya vifaa vya matengenezo ya ndege.

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Allan Kilavuka alisema shirika hilo limepata ugumu wa kupata vifaa vinavyohitajika kwa baadhi ya ndege zake zinazofanyiwa matengenezo.

Alisema shirika hilo la ndege linaweza kulazimika kupunguza baadhi ya safari iwapo changamoto zitaendelea.

Alilaumu vita vya Russia na Ukraine kwa tatizo hilo, ambalo alisema limeathiri usafirishaji wa malighafi muhimu za Urusi katika sekta ya anga.

"Changamoto zimesababishwa na mzozo wa vita vya Ukraine ambao umeathiri kwa kiasi kikubwa usambazaji wa bidhaa muhimu kwa usafiri wa anga duniani kutoka Urusi," alisema.

Hivyo mashirika ya ndege yamelazimika kutafuta kote duniani kupata vifaa wanavyovihitaji."

Shirika la ndege la Kenya Airways ambalo ni miongoni mwa mashirika makubwa ya ndege barani Afrika, linatumia ndege za Boeing na Embraer.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live