Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhaba wa mafuta Tigray wakwamisha misaada

Mafuta Pc Data Uhaba wa mafuta Tigray wakwamisha misaada

Sun, 24 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku ya nne tangu Kikosi cha Anga cha Jeshi la Ethiopia kilipoanza kushusha makombora katika Jimbo la Tigray, Umoja wa Mataifa umesema mashirika yanayosambaza chakula mjini humo, yanashindwa kuendelea na wajibu wao kutokana na uhaba wa mafuta.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu sambazaji wa misaada hiyo ya kibinadamu, imesema uhaba huo wa mafuta umetokana na kuzuiwa kwa zaidi ya malori 14 katika Mkoa wa Afar, njia kuu ya kuingilia Tigray ingawa yamepewa kibali cha kuendelea na safari.

“Kutokana na uhaba mkubwa wa mafuta, mashirika mengi ya misaada yamesitisha huduma,” umesema umoja wa Mataifa kwenye ripoti yake ya wiki.

Umoja huo umesema tangu Oktoba 11, kati ya mashirika saba yaliyopo, matatu yamelazimika kusitisha usambazaji wa chakula na manne yaliyobaki hayatosambaza nje ya Mekele baada ya wiki moja iwapo hali itaendelea kuwa hivi.

Mapigano kati ya askari wa chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF) cha Jimbo la Tigray na Jeshi la Ethiopia yaliibuka Novemba mwaka jana. Mpaka mwishoni mwa Juni, TPLF ilikuwa imeichukua miji muhimu ya jimbo hilo yakiwamo makao makuu yake, Mekele.

Tangu kuzuka kwa mapigano hayo, maelfu ya raia wameyakimbia makazi yao huku waliobaki akikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

Wiki iliyopita, Umoja wa Mataifa ulisema idadi ya watoto wadogo waliolazwa kutokana na kukosa lishe bora kati ya Februari na Agosti imeongezeka maradufu ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kipindi kama hicho mwaka jana.

Ripoti iliyotolewa juzi pia ilieleza kuwa mpaka wiki iliyoishia Oktoba 13 ni watu 52,000 pekee walipokea msaada wa chakula jimboni Tigray sawa na asilimia moja tu ya zaidi ya watu milioni 5.2 waliopo.

“Kuwafikiwa watu milioni 5.2 ndani ya wiki sita, mashirika yanatakiwa kutoa chakula kwa wastani wa watu 870,000 kila wiki,” inasema ripoti hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live