Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhaba wa madaktari wasababisha majanga Nigeria

Doctorrrrrrr Uhaba wa madaktari wasababisha majanga Nigeria

Mon, 19 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nigeria, nchi yenye zaidi ya watu milioni 220, ina madaktari 10,000 pekee, suala ambalo linawafanya wagonjwa wakabiliwe na matatizo mengi katika kupata huduma za matibabu.

Mohammad Nur Ghazali, mkuu wa ofisi ya Chama cha Madaktari wa Nigeria huko Bauchi, amesema: Kulingana na ripoti ya Shirika la Afya Duniani, daktari mmoja anapaswa kutoa huduma kwa wagonjwa 600 katika kila nchi lakini hali ni kinyume chake nchini Nigeria.

Ghazali amesema, nchini Nigeria ambayo ina watu zaidi ya milioni 220, daktari mmoja hutembelea wagonjwa zaidi ya 9,000, na idadi ya madaktari katika nchi hii ni 10,000 tu. Amesisitiza kuwa madaktari wengi wa nchi hiyo wamehamia Marekani, Saudi Arabia, na nchi za Ulaya.

Mkuu wa ofisi ya Chama cha Madaktari wa Nigeria huko Bauchi amesema mambo mengi yanasababisha kuhama kwa madaktari kutoka Nigeria na kwenda ng'ambo, na muhimu zaidi ni mishahara duni ya madaktari iliyowalazimisha wengi kuhamia nje ya nchi.

Wanigeria wengi wanaamini kwamba iwapo serikali ya shirikisho ya nchi hiyo itatayarisha mazingira ya ushindano kwa ajili ya kazi ya madaktari kama ilivyo katika nchi zingine, wanataaluma hao hawatalazimika kuhama nchi yao na kwenda ng'ambo ili kupata kipato kikubwa zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live