Waziri wa biashara wa Kenya Moses Kuria amesema kuwa uhaba wad ola nchini humo umeshindwa kudhibitiwa na serikali.
Bw Kuria aliwaambia wabunge Jumatano kwamba uhaba wad ola unaikabili dunia nzima lakini akalaumu utamaduni wa Kenya wa kuagiza vitu nje ambavyo vinaweza kutengenezwa ndani ya nchi.
Huwezi kuwa unalia kwamba tuna matatizo na dola wakati tunaagiza kila kitu ," alisema.
Alitoa wito wa kutolewa motisha ili kuwatia moyo wazalishaji wa bidhaa nchinina kuwalinda na washindani wa kigeni.
Benki kuu ya Kenya (CBK) imeyaabiza mabenki ya kibiashara kuwa na mgao wa zamu wad ola kufuatia uhaba wa sarafu hiyo, vimeripoti vyombo vya habari nchini humo.
Wachambuzi wameilaumu CBK kwa mzozo wa dila, wakisema benki hiyo ilianzisha sheria kali katika soko la fedha kati ya mabenki.
Lakini benki hiyo imekuwa ikisema kuwa kenya ina akiba ya kutosha ya fedha za kigeni kukidhi mahitaji.
Shilingi ya Kenya imepoteza 9% dhidi yad ola ya kimarekani katika kipindi cha mwaka mmoja, na hivyo kusababisha kupanda kwa garama ya maisha.