Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ugonjwa wa 'Red Eyes' waripotiwa Kenya

Red Eyesss (25).jpeg Ugonjwa wa 'Red Eyes' waripotiwa Kenya

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wataalam wa afya nchini Kenya wanachunguza mlipuko wa maambukizo ya ugonjwa wa macho mekundu “Red eyes”, unaowasumabua wakaazi wa jiji la Mombasa na Kilifi pwani ya nchi hiyo.

Wakazi wameshauriwa kuzingatia kanuni za usafi kama vile kunawa mikono, kuepuka kushiriki vitu vya kibinafsi na kuacha kugusa macho yao.

Wiki iliyopita, mamlaka za afya nchini Tanzania zilitoa tahadhari baada ya kurekodi visa 869 vya ugonjwa huo katika mwezi mmoja, wengi wao wakiwa katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam.

Conjunctivitis, pia inajulikana kama ugonjwa mwekundu wa jicho ambapo pia unaifanya sehemu inayolinda macho kuvimba .

Ugonjwa husababishwa na mzio au maambukizi na dalili zake ni kama vile macho kuwa mekundu, uvimbe, machozi au kuwasha.

Wagonjwa wengine wanaweza pia kutoa uchafu kutoka kwa jicho kwa mujibu wa maofisa wa afya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live